KINDA MZALIWA WA KIGOMA ASAJILIWA BUYERN MUNICH

Kinda mwenye umri wa miaka 17, Nestory Irankunda ( wa pili kushoto) mzaliwa wa mkoa wa Kigoma, amesajiliwa na mabingwa wa kihistoria wa Ujerumani, Buyern Munich.

Irankunda, ambaye wazazi wake wana asili ya Burundi, alizaliwa katika Kambi ya Wakimbizi mkoani humo na kwa sasa anaishi Australia, akiichezea klabu ya Adelaide United.

Katika usajili huo, kinda huyo ambaye tayari ameshazichezea timu za taifa za vijana za Australia, amenunuliwa kwa dau la pauni milioni 3, sawa na shilingi bilioni tisa na atajiunga na timu hiyo Julai Mosi mwakani.

No comments