KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YAIPONGEZA DAWASA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI


 Na Asheri Bernard Mfaume


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imeipongeza mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Pwani na Dar Es Salama (DAWASA) baada ya kukagua miradi ya Wami - Ruvu  uliogharimu Billion 160.7, Mradi wa kusukuma Maji Tegeta A na Goba wenye thamani ya Billion 17 na mradi wa Maji taka Mbezi Beach na Salasala wenye thamani ya Billion 128.

Akizumgumza na wandishi wa Habari  kwa niaba ya Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Deus Clement Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela, amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka Fedha nyingi katika Sekta Maji. Pia ameipongeza Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya Dawasa kwa usimamizi Mzuri wa miradi hiyo.

Aidha, Kamati imetoa Rai kwa Taasisi Zote zilizo chini ya Wizara ya maji zinazotekeleza miradi mbalimbali hapa nchini kuwa na weledi ili lengo la Serikali la kuwafikishia wananchi Maji vijijini liweze kutimia kwa wakati.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete, ameiomba Kamati hiyo iendelee kuweka msukumo kwa Serikali ili fedha za usambazaji wa maji kiasi Cha Billion 1.8 katika ngazi ya kaya ziweze kupelekwa Jimboni Chalinze.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa, Gen Mstaafu Davis Mwamunyange ameishukuru Kamati kwa kutembelea Miradi hiyo na kuahidi kusimamia menejimenti ili maelekezo yote ya kamati yaweze kufanyiwa kazi.


No comments