Hamas inasema uvamizi wa Al-Shifa ni 'uhalifu dhidi ya binadamu'
Ofisi ya habari vya serikali ya Hamas imetoa taarifa ikiutaja uvamizi wa Israel katika hospitali ya Al-Shifa ya Gaza kuwa ni "uhalifu wa kivita", "uhalifu wa kimaadili" na "uhalifu dhidi ya binadamu".
Ilisema wagonjwa 9,000, wahudumu wa afya na raia walioyakimbia makazi yao walikuwa hospitalini wakati uvamizi huo uliofanyika usiku.
Katika video kwenye X, (zamani ikiitwa Twitter,) na Kituo cha Habari cha Palestina, kiongozi wa Hamas Izzat al-Rishq alisema Israeli ilishambulia kituo cha kiraia, sio eneo la kijeshi.
Katika taarifa ya awali, Hamas ilisema inaiwajibuisha Washington na rais wa Marekani Joe Biden kuhusika na uvamizi huo.
Israel na Marekani zinadai kuwa Hamas lina kambi yake chini ya hospitali kuu ya Al-Shifa, jambo ambalo Hamas inakanusha.

Post a Comment