Mahakama Korea Kusini yapiga marufuku mapenzi ya jinsia moja jeshini
Mahakama ya kikatiba ya Korea Kusini imegongelea msumari sheria inayopiga marufuku mahusiano ya jinsia moja katika jeshi, katika kile wanaharakati wamekiita kurudisha nyuma haki za LGBT.
Mahakama ilisema uhusiano wa jinsia moja unaweza kudhuru utayari wa wanajeshi na kudhoofisha nidhamu.
Kujamiiana kwa jinsia moja kati ya raia hata hivyo, sio uhalifu.
Huduma ya kijeshi ni ya lazima nchini Korea Kusini, huku wanaume wote wenye umri kati ya 18 na 28 wanatakiwa kuhudumu kwa takribani miezi 20.
Wanaharakati walilaani uamuzi huo, wakisema unachochea ghasia na ubaguzi dhidi ya askari wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja.
Marufuku hiyo "imeanzisha ubaguzi, imeimarisha hasara za utaratibu zinazowakabili watu wa LGBT na kuhatarisha kuchochea au kuhalalisha unyanyasaji dhidi yao, ndani ya jeshi na katika maisha ya kila siku", mtafiti wa Amnesty International Mashariki mwa Asia Boram Jang alisema katika taarifa.
Mahakama iliamua kwamba kifungu cha 92-6 cha kitendo cha uhalifu wa kijeshi kilikuwa cha kikatiba. Kitendo hakirejelei kwa uwazi ngono ya watu wa jinsia moja bali kinapiga marufuku "kufanya ngono kwa njia ya kinyume na maumbile" au "tendo lingine lolote lisilofaa".
Ndoa ya watu wa jinsia moja haitambuliwi nchini humo na kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakati mwingine huonekana kama ulemavu au hata changamoto ya kiafya nchini Korea Kusini.

Post a Comment