vita vya Gaza: Biden aionya Iran katika ujumbe adimu wa moja kwa moja
Ikulu ya White House inasema Joe Biden ameionya Iran dhidi ya kuwalenga wafanyakazi wa Marekani katika Mashariki ya Kati, kupitia ujumbe adimu kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
"Kulikuwa na ujumbe wa moja kwa moja uliotumwa," msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la White House John Kirby alisema katika mkutano mapema leo.
Hakutoa maelezo zaidi. Pentagon pia ilisema takribani wanajeshi 900 wa ziada wa Marekani wako katika eneo hilo au wameelekea huko ili kuimarisha ulinzi wa anga ili kuwalinda wafanyakazi wa Marekani, huku kukiwa na ongezeko la mashambulizi katika eneo hilo.
Wanajeshi wa Marekani wameshambuliwa takribani mara 12 nchini Iraq na mara nne nchini Syria katika wiki iliyopita, kwa mujibu wa Pentagon.
Mapema wiki hii, Biden alisema alikuwa amemuonya Ayatollah kwamba Marekani ingejibu ikiwa vikosi vyake vitaendelea kulengwa. Hakufafanua jinsi ujumbe huo ulivyowasilishwa.

Post a Comment