WAZIRI MCHENGERWA AKOSHA WATUMISHI MALIASILI NA UTALII
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa jana aliwakosha watumishi wa wizara hiyo wakati akitoa nasaha zake kwenye kikao cha 30 cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo, aliposema angetamani kukutana na kila mtumishi ili aweze kujua kero yake.
Maneno hayo yalionekana kuwakosha watumishi hao ambao kwa nyakati tofauti walisema kwamba kuna kero nyingi kwao ikiwa ni pamoja na mabosi kujipangia safari za semina, warsha na makongamano, ambazo kimsingi zilipaswa kuhudhuriwa na maofisa wa chini.
"Utakuta mameneja wanakwenda kuhudhuria semina au warsha ambazo walipaswa kwenye field officers, wanakwenda labda siku tano, wanachukua posho na wakirudi ofisini wanawaita hao maofisa na kuwafundisha kwa muda .mchache kile walichokipata kwenye semina," alisema ofisa mmoja wa ngazi ya chini aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Alisema watumishi wangependa kumuona Waziri Mchengerwa akitengeneza utaratibu wa kuonana na watumishi, hasa wa ngazi ya chini, kwani wana mengi ya kumwambia.

Post a Comment