RAIS SAMIA ASEMA SERIKALI IMEKUSUDIA KULETA MAGEUZI YA KILIMO TANZANIA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imekusudia kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kiweze kuchangia pato la taifa tofauti na ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Ikulu kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Zuhura Yunus, Rais Samia alitoa wito huo wakati akizindua mpango wa mashamba makubwa ya pamoja (Block Farming) huko Chinangali wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Aliwataka wadau wa kilimo kushirikiana na Wizara ya kilimo pamoja na wataalam wa kilimo ili kubuni miradi itakayoleta tija kwa taofa.

Licha ya kuzindua mpango huo, pia Rais Samia alikabidhi mitambo na magari kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kutaka mazao, uvuvi na ufugaji kuchangia ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 3.6 ya sasa hadi kufikia asilimia 10 ifikapo 2030.

Mpango huo unaojulikana kama Jenga Kesho iliyo Bora (Build Better Tomorrow) tayari imetenga eka 400 mkoani Dodoma na kwamba zipo eka 47000 katika mikoa mingine ambako wataalamu wanapima udongo ili kujua aina ya virutubishi vinavyotakiwa.

Rais serikali kwa kupitia wizara ya kilimo imejidhatiti kuhakkkisha mpango huo unafikia malengo.

Aidha Rais Samia alimtaka Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kusimamia fedha zilizotolewa kwenye mradi huo ili kuhakiisha hakuna ubadhilifu unaofanyika.

No comments