POLISI WATOA ELIMU WEZI WA MITANDAO YA SIMU, SOMA HAPA UJUE MBINU ZAO
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendesha semina kwa maofisa wa Polisi Jamii na Polisi Kata juu ya mbinu mpya za matapeli wa simu na mikononi, baada ya mtindo wa Tuma kwa Namba Hii kubuma kufuatia kuboreshwa kwa mfumo unaowashinda wezi hao.
Msemaji wa Jeshi la Polisi David Masime akiwa katika semina hiyo ambayo inawashirikisha pia maofisa kutoka Wilaya za Mkuranga na Kibaha, alisema matapeli hao hivi sasa wamegeukia kujifanya kuwa mawakala wa kusajili laini, kurudisha namba zilizopotea na kusajili laini mpya.
Alisema wapo mawakala halali wa mitandao ya simu wanaozunguka mitaani, lakini pia ndani yao wapo matapeli ambao tofauti yao ipo kwa namna ya utendaji wao wa kazi.
"Ukiona wakala anakuambia toa line yako nipe nikuunge na vifurushi vya chuo, ujue huyo ni tapeli, hata anapokuambia ingiza namba yako ya siri halafu anageukia pembeni, anakudanganya tu, kwani wana uwezo wa kudukua mawasiliano yako na pia unapoingiza namba zako zinabaki katika simu zao," alisema.

Post a Comment