URUSI YAUSAMBARATISHA MJI WA BARKUMUT KWA MAKOMBORA
Vikosi vya jeshi la Urusi ambavyo vimeadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzisha mashambulizi yake kwa Ukraine, leo imeshambulia vikali kwa makombora katika mji wa Barkumut kiasi cha kuharibu miundombinu na kuleta hasara kubwa.
Urusi imefanya mashambulizi hayo huku ikijua kwamba mkutano wa nchi tajiri duniani maarufu kama G 20, unaofanyika nchini India utabeba ajenda ya kuilaani nchi hiyo kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine, inayoungwa mkono na Nchi wanachama wa Umoja wa kujihami Ulaya, NATO.
Aidha, mkutano huo unafanyika kukiwa na vuguvugu la mgogoro kati ya Marekani na China, ambazo hazina uhusiano mzuri tangu Marekani ilipoyatungua maputo yanayodaiwa kuwa ya kijasusi ya China.

Post a Comment