MIAKA KUMI IJAYO ASILIMIA 39 YA KAZI ZA NYUMBANI ZITAFANYWA NA ROBOTI

.


Ndani ya muongo Ndani ya muongo mmoja, karibu asilimia 39 ya wakati unaotumika kwa kazi za nyumbani na kutunza wapendwa inaweza kuwa otomatiki, kulingana na wataalam.

Watafiti kutoka Uingereza na Japan waliuliza wataalam 65 wa akili bandia (AI) kutabiri kiwango cha uwekaji kiotomatiki katika kazi za kawaida za nyumbani miaka kumi kutoka sasa.

Wataalamu walitabiri kuwa ununuzi wa mboga unaweza kuwa wa kiotomatiki zaidi, wakati kutunza watoto au wazee kunaweza kuathiriwa na AI.

Utafiti huu umechapishwa katika jarida la PLOS ONE.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oxford na Chuo Kikuu cha Ochanomizu nchini Japani walitaka kujua roboti zinaweza kuwa na athari gani kwa kazi ya nyumbani isiyolipwa: "Ikiwa roboti zitachukua kazi zetu, je, pia zitapeleka nje takataka badala yetu?" waliuliza.

Roboti "za kazi za nyumbani", kama vile za kufanya usafi, "zimekuwa roboti zinazozalishwa zaidi na zinazouzwa zaidi ulimwenguni", watafiti walisema.

Timu iliuliza wataalam 29 wa AI kutoka Uingereza na wataalam 36 wa AI kutoka Japani kuhusu utabiri wao wa roboti nyumbani.

Watafiti waligundua kuwa wataalam wa kiume wa Uingereza walielekea kuwa na matumaini zaidi kuhusu mitambo ya kiotomatiki ya nyumbani kuliko wenzao wa kike, hali iliyobadilika nchini Japani.

Lakini kazi ambazo wataalam wanafikiria kuwa mfumo wa otomatiki unaweza kutekeleza zinatofautiana: "Ni asilimia 28 tu ya kazi ya utunzaji, pamoja na shughuli kama vile kufundisha mtoto wako, kuandamana na mtoto wako au kumtunza jamaa mzee, inapaswa kufanywa kiotomatiki," anasema Dk Lulu Shi, mtafiti huko Oxford Internet Institute .

Kwa upande mwingine, teknolojia inapaswa kupunguza muda tunaotumia kwa ununuzi kwa asilimia 60, kulingana na wataalam.

Lakini utabiri kwamba "ndani ya miaka kumi" roboti zitatukomboa kutoka kwa kazi za nyumbani zina historia ndefu na wasiwasi fulani unaweza kuthibitishwa. Mnamo 1966, kipindi cha Televisheni cha Tomorrow's World kiliangazia roboti ya nyumbani ambayo inaweza kupika chakula cha jioni, kumtembeza mbwa, kumtunza mtoto, na kazi zingine nyingi.

Ikiwa waundaji wake wangepata pauni milioni 1 tu, kifaa hicho kingeweza kufanya kazi mnamo 1976, kulingana na ripoti...

 

 

No comments