GODBLESS LEMA AWASILI ARUSHA, MAMIA YA WAFUASI WAFURIKA UWANJANI

Mamia kwa mamia ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia  na Maendeleo (Chadema) leo walijazana katika uwanja wa ndege wa KIA, kumpokea Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema, akitokea nchini Canada.

Lema alikimbilia Canada mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 kwa kile alichodai kuhofia usalama wake,akipitia Nairobi nchini Kenya akiwa ameambatana na familia yake.

Wafuasi wa Chadema, wakiwa wanapeperusha bendera za chama hicho, waliruhusiwa kuingia ndani kabisa ya uwanja kumlaki mwanasiasa huyo wa pili wa chama hicbo kurejea baada ya kuomba hifadhi ya ukimbizi huko ughaibuni.

Wa kwanza alikuwa ni bosi wake, Tundu Lissu ambaye alielekea Ubelgiji lakini naye akarejea nchini hivi karibuni baada ya kuwepo kwa maridhiano ya kitaifa kufuatia uamuzi wa Rais Samia kuunda kikosi kazi cha kuangalia maeneo ya kuliponya taifa.

No comments