URUSI, CHINA NA IRAN WAMALIZA ZOEZI LA PAMOJA LA KIJESHI BAHARI YA ARABIA
Huku vita kati ya Urusi na Ukraine ikiendelea katika mwaka wake wa pili, nchi hiyo ya Kisovieti imemaliza mazoezi ya siku tatu ya kijeshi kati yake na washirika China na Iran.
Nchi hizo tatu ambazo zinaangaliwa kwa umakini na Marekani kama tishio kwa usalama wa dunia, zilifanya mazoezi hayo katika Bahari ya Arabia kwenye pwani ya Chandahar nchini Iran.
Rais Vladimir Putin wa Urusi na Xi Jimping wa China, wamesema mazoezi hayo yalikuwa ni ya mafanikio makubwa na kwamba hayataathiri usalama wa dunia.
Jimping anajiandaa kwa ziara ya kiserikali nchini Urusi na mipango yake ni kuona jinsi ya kumaliza vita hivyo, jambo ambalo White House, Ikulu ya Marekani imesema haiamini.

Post a Comment