ABEL AMROUCHE AKUTANA NA KAPOMBE, SHABALALA BAADA YA MECHI YA HOROYA

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Abel Amrouche, usiku huu amekutana na kuzungumza na walinzi wawili wa pembeni wa Simba, aliowaacha katika kikosi alichokiita kambini, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein Shabalala.

Katika video inayosambaa mitandaoni hivi sasa, kocha huyo mgeni ambaye uteuzi wake wa wachezaji unapingwa na baadhi ya wadau katika maeneo kadhaa, ikiwemo kuwaacha walinzi hao wazoefu na bora kwa sasa, alionekana akizungumza nao wakiwa watatu tu.

Walinzi hao waliiongoza Simba usiku huu kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya kutoka Guinea katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambako Simba imefuzu kwa robo fainali.

Bado haijafahamika aliongea nao nini lakini wawili hao hawamo katika orodha ya wachezaji wa Stars walioitwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda, kuwania kufuzu kwa fainali za Afcon mwaka huu.

No comments