UGANDA YAIVIMBIA MAREKANI KUHUSU USHOGA, YASEMA MSITUINGILIE

Wakati Marekani, moja kati ya mataifa ya nje yanayotoa msaada mkubwa kwa nchi ya Uganda ikitoa onyo la kuitaka kutosaini sheria ya kuwahukumu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Rais Yoweri Museveni ametia saini muswada wa sheria unaowapeleka jela miaka kumi hadi maisha wapenzi wa jinsia moja.

Awali, Marekani ilitoa onyo la kusitisha misaada yake kwa Uganda endapo Uganda ingesaini sheria hiyo, lakini Museveni, mmoja kati ya viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi Afrika, aliwaita waandishi wa habari wa ndani na nje ya kutia saini muswada huo mbele yao.

"Hii ni nchi yetu, hatutaki watu watuingilie mambo yetu ya ndani, tuna utamaduni wetu, haturuhusu aina hiyo ya maisha." Museveni aliwaambia wanahabari.​

No comments