SIMBA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA, MTU ALA WIKI LUPASO

Clatous Chota Chama, mchezaji fundi zaidi katika kikosi cha Simba, usiku huu ameiongoza timu hiyo kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuirarua Horoya kutoka Guinea kwa kichapo cha mabao 7-0 huku yeye akitupia mabao matatu.

Simba ambayo ilipigwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Conakry, mji  mkuu wa Guinea, leo ilitakata kila idara, ikienda mapumziko kwa ushindi wa mabao 3, mawili yakifungwa na mwamba wa Lusaka, moja kwa mpira wa adhabu nje ya 18, na baadae kwa penati.

Kwa ushindi huo, wachezaji wa Mnyama wamechukua milioni 250 walizoahidiwa na bodi ya wakurugenzi, achilia mbali milioni 35 kutoka kwa Mama wa Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kesho ni zamu ya mabingwa wa nchi, Yanga ambao nao watahitaji ushindi ili kuingia robo fainali ya kombe la shirikisho, wakiwakaribisha Monastry ya Tunisia.

No comments