MUASISI WA CHADEMA AZIKWA LEO JIJINI MWANZA, MBOWE,MNYIKA KUONGOZA
Mmoja wa waasisi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sylivester Masinde, aliyefariki Machi 15 mwaka huu katika Hospitali ya Bugando amezikwa leo jijini Mwanza.
Masinde ambaye alilazwa kwa muda katika hospotali hiyo ya Rufaa, amezikwa na umati mkubwa wa wananchi pamoja na wanachama wa chama chake, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
Pia Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu pia walihudhuria mazishi hayo.
RIP Mzee Masinde.

Post a Comment