ANAYELAWITI WATOTO MAGOMENI ANADUNDA TU MITAANI BILA WASIWASI
Wakati Afrika ikiwa katika mjadala mkubwa wa kupinga mapenzi ya jinsia moja, pale Magomeni jijini Dar es Salaam, kijana mmoja anayefahamika kwa kuwalawiti watoto, anadunda tu mtaani bila hofu, licha ya vitendo vyake hivyo kufahamika hadi kwa viongozi wa serikali ya mtaa.
Mama mmoja wa mtoto mwenye umri wa miaka nane (majina yao yanahifadhiwa), amekiambia kituo kimoja cha tv kuwa kijana huyo amemlawiti mara sita na anafahamika, lakini hakamatwi.
Habari hizo zilithibitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpakani katika Kata ya Ndugumbi, Musa Mwingwa akisema serikali inafahamu juu ya vitendo vinavyofanywa na kijana huyo lakini haelewi kwa nini hakamatwi.

Post a Comment