PAC YARIDHISHWA UJENZI WA BARABARA NJOMBE-MORONGA
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Wizara
ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Balozi, Eng. Aisha Amour wakati kamati
hiyo ilipokagua barabara ya Njombe-Moronga KM 53.9 ambayo ujenzi wake kwa kiwango
cha lami umekamilika.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeelezea kuridhishwa kwake na kazi ya ujenzi wa barabara mkoani Njombe.
Makamu Mwenyekiti wa
kamati hiyo Mhe. Japhet Hasunga amesema baada ya kupitia na kukagua barabara ya
Njombe-Moronga KM 53.9 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika
wameridhika na utekelezaji wa mradi huo.
“Nitoe wito kwa
watumiaji wa barabara kuhakikisha wanazingatia alama za barabarani na maelekezo
mengine halali ili kuepusha ajali na kuwezesha barabara kudumu kwa muda uliokusudiwa”, amesema Mhe.
Hasunga.
Mkuu wa mkoa wa Njombe
Anthony Mtaka ameishukuru Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kutoa fedha zaidi ya
bilioni 5 ili kuwezesha kujengwa kwa barabra kuelekea eneo la Liganga na Mchuchuma
na kusema hatua hiyo itawezesha uwekekezaji mkubwa wa chuma na makaa ya mawe na
hivyo kukuza uchumi wa mkoa huo.
“Tunaishukuru
Serikali kwa ujenzi wa barabara za lami za kimkakati hali itakayovutia
wawekezaji wa kilimo, utalii na viwanda mkoani humu,” amesema Mtaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi
na Uchukuzi Balozi, Eng. Aisha Amour ameishukuru kamati ya PAC na kuahidi Wizara
itatekeleza maelekezo yake ili kuboresha miradi inayoendelea na hivyo kuleta
tija kwa wakati.
Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iko mkoani Njombe kukagua utekelezaji wa
miradi ya Serikali ambapo pamoja na mambo mengine imekagua barabara ya
Njombe-Moronga KM 53.9 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI.

Post a Comment