MTANDAO WA MAJASUSI WA URUSI WAKAMATWA POLAND


Watu sita wanaodaiwa kuwa majasusi wa Urusi wamekamatwa nchini Poland, wakidaiwa kufunga kamera kuchunguza miundombinu inayotumiwa na nchi hiyo kusafirisha misaada ya kijeshi na kibinadamu kwa Ukrane wakiwa na lengo la kuifanyia hujuma, maafisa wa serikali wameiambia BBC.

RMF FM ilisema kuwa kikundi hicho kilikuwa kimeandaa mipango ya hujuma katika wakati ambao mzozo wa kijasusi kati ya Urusi na nchi za Magharibi ukiwa unazidi hasa baada ya kuanza kwa vita kati yake na Ukraine.

Poland ni mojawapo ya washirika wakuu na vikosi vyake vimemekuwa vikiwakamata watu kadhaa wanaoshukiwa kufanya ujasusi kwa ajili ya Urusi tangu ianze uvamizi Februari mwaka jana.

Kulingana na kituo hicho cha redio, kikundi hicho cha majasusi kilikuwa kimeweka kamera za video CCTV kando ya makutano ya njia ya leri na barabara muhimu ya usafirishaji iliyopo katika jimbo la Poland la Podkarpackie , inayopakana na Ukraine, ilisema

Baadhi ya kamera hizo zilipatikana zimewekwa karibu na kiwanja kidogo cha mkoa cha ndege ambacho kimegeuzwa kuwa cha kimataifa kwa ajili ya kusafirisha misaada ya kijeshi na ya kibinadamu kwa Ukraine.

No comments