INJINIA HERSI AKUTANA NA BALOZI WA HISPANIA NCHINI, AIPA DOLE LALIGA
Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amekutana na Balozi wa Hispania nchini Tanzania, Mheshimiwa Jorge Moragas nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Katika akaunti yake ya Twitter, aliandika: "Imekuwa siku njema kukutana na Balozi wa Uhispania nchini Tanzania katika makazi yake jijini Dar es Salaam.
Nimemshukuru kwa ushiriki wa @laliga katika transformation project yetu na sasa tunaanza kuona matunda yake."


Post a Comment