MLIPUKO NA MOTO MKUBWA KATIKA JENGO LA URUSI, KM 75 KUTOKA UKRAINE
Mlipuko mkubwa na moto umerekodiwa katika jengo linalotumika kuhifadhia silaha la FSB lililoko katika jiji la Rostov-on- Don, umbali wa km 75 kutoka uwanja wa vita nchini Ukraine.
Wenyeji wa jiji hilo walisema walisikia milipuko kabla ya jengo hilo kuwaka moto na video zilizorushwa zilionyesha moto mkubwa uligubikwa na moshi ukiwaka kwa nguvu, kwa mujibu wa shirika la habari la Tass,
Mashuhuda walisema ghala hilo linalohifadhi risasi liliwaacha watu wawili wakiwa wamejeruhiwa na milipuko ilikuwa ikisikika kila baada ya sekunde kumi, lakini hakukuwa na uhusiano wowote na shambulizi kutoka Ukraine.


Post a Comment