BURNA BOY HAKAMATIKI, SASA KUFANYA VITU VYAKE FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Damini Ebunoluwa Ogulu,ambaye ni maarufu zaidi duniani kwa jina la kisanii la Burna Boy, atatumbuiza wakati wa mchezo wa fainali za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, itakayopigwa katika dimba la Ataturk Olympic jijini Istanbul nchini Uturuki, Juni 10 mwaka huu.

Burna Boy ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Grammy kutoka nchini Nigeria,  ametangazwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza katika fainali hizo za mwaka huu na Shirikisho la soka barani (UEFA) Ulaya lilithibitisha Alhamisi asubuhi.

“Habari kubwa! @burnaboy atakuwa akitumbuiza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Istanbul pamoja na kichwa kingine cha ajabu!” ilisema taarifa ya UEFA yenye video ya kicheshi ya kijana huyo anayejiita ‘African Giant’.

Mkali mwingine wa Nigeria, Davido alitumbuiza kwenye fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 mbele ya zaidi ya mashabiki 80,000 kwenye Uwanja wa Lusail Iconic, Qatar.

No comments