MIZENGO PINDA ATEULIWA MWENYEKITI WA KUMSHAURI RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Rais Samia Suluhu Hassan leo amemteua Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Kayanza Pinda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kumshauri Rais kuhusu utekelezaji wa masuala ya Kilimo na Chakula.
Katika uteuzi huo ambao utazinduliwa Ijumaa hii Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia amemteua Dkt. Jacqueline Mkindi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticulture Association (TAHA) kuwa mjumbe wa Sekretarieti ya Baraza la Kumshauri Rais kuhusu kilimo na chakula.
Wajumbe wengine wa Baraza hilo waliotangazwa leo ni Dkt Florence Turuka na Dkt. Mwatima Juma.

Post a Comment