MFAUME MFAUME, IDDI PIARALI NUSURA WAZICHAPE KAVUKAVU LEADERS CLUB LEO

Rais wa TPBRC, Chaurembo Palasa akiamua ugomvi wakati Mfaume na Piarali walipotaka kuchapana mchana huu Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Mabondia Mfaume Mfaume na Iddi Piarali, ambao walizichapa Desemba mwaka jana jijini Arusha na pambano lao kushindwa kumalizika kwa sababu za kiufundi, almanusra wazichape kavukavu leo walipokutana katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es  Salaam mchana huu.

Wawili hao walikutanishwa hapo na promota kutoka kampuni ya PQPB ambao wanataka pambano hilo lililosimamishwa kwa sababu ya mabondia hao kugongana vichwa na kuumia, lirudiwe Septemba mwaka huu.



Mabondia hao ambao wamejenga uhasimu mkubwa katika siku za karibuni, ni majirani wakiishi Manzese anakotokea Piarali na Mabibo,nyumbani kwa Mfaume.


Iddi Piarali akiingia katika eneo la utambulisho akiwa amebebwa mabegani huku mamia ya mashabiki zake wakishangilia.



Mfaume Mfaume akiwa amezungukwa na mashabiki wake wakati akiingia katika eneo la utambulisho, akiwa anesimama kwenye gari lililomleta akifunikwa mwavuli kumkinga na jua kali la Dar es Salaam.


Piarali akiingia eneo la tukio


Mashabiki wa Piarali wakishangilia wakati akiingia.


Mashabiki wa Mfaume Mfaume wakimshangilia





No comments