MAREKANI YASEMA UZEMBE WA MARUBANI WA URUSI ULISABABISHA KUANGUSHA NDEGE YAO

Marekani imeishutumu Urusi kwa tabia ya uzembe baada ya ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani kuanguka ndani ya Bahari Nyeusi kufuatia kugongana na ndege za mapigano za Urusi.

Kabla ya kugongana, ndege za mapigano aina ya jet za Urusi zinasemekana kumwaga mafuta katika njia ya droni, ambayo Marekani inasema ilikuwa ni njia ya safari za anga za kimataifa.

Droni ya MQ-9 Reaper iliangushwa Jumanne baada ya makabiliano yaliyodumu kwa muda wa dakika kati ya 30-40, Marekani ilisema.

Urusi inakanusha kwamba ndege zake mbili za mapigano aina ya jet Su-27 zilifanya mawasiliano.

Swali muhimu linaloulizwa ni iwapo mgongano ulikua ni jaribio la Urusi la kuvuruga droni ya Marekani na kazi yake- au iwapo lilikuwa ni jaribio la kuiangusha chini.

Maafisa wa kijeshi wa Marekani wanasema tukio hillo lilitokea saa moja na dakika 3(06:03 GMT) Jumanne.

Mara kadhaa kabla ya mgongano, jest za kivita ziliangusha mafuta kwenye droni"kiuzembe, bila kujali mazingira na kwa uzembe , bila maadili ya kitaaluma", ilisema taarifa hiyo.

Iliongeza kuwa : "ndege zetu za MQ-9 zilikuwa katika operesheni yake ya kawaida katika anga la kimataifa ilipopigwa na ndege ya Urusi, na kusababisha kuanguka na kupotea kabisa kwa MQ-9."

Katika jibu lake kwa Marekani, Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa droni ilianguka baada ya 'kukwepa kwa ujanja' na kuongeza kuwa droni ya MQ-9 Reaper ilikuwa inasafiri huku Transponders zake zikiwa zimezimwa. Transponders ni vifaa vya mawasiliano vinavyoruhusu ndege kufuatiliwa.


No comments