MBUNGE DITOPILE AFUTURISHA DODOMA, WAMUOMBEA DUA RAIS SAMIA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Mariam Ditopile ameandaa Iftari na Dua Maalum ya Watoto Yatima na Wajane kuiombea nchi na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika muendelezo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Hafla hiyo ya Iftari imefanyika katika Hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma  ambapo Mgeni wa Heshima alikua ni Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo, ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini David Kihenzile. 

Mbunge huyo wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile, licha ya kuwatufurisha waislamu hao, amewatakia Ramadhani njema waislamu wote nchini.

No comments