AKINA MAMA DODOMA WAMPA TUZO MBUNGE MAVUNDE KWA KUWAWEZESHA KIUCHUMI

Jukwaa la Wajasiriamali Mkoa wa Dodoma limemkabidhi tuzo ya shukrani Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mheshimiwa Anthony Mavunde kwa uwezeshaji wake kiuchumi kwa kundi hili la akinamama kupitia programu mbalimbali anazoziendesha katika Jiji la Dodoma.

Tuzo hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa niaba ya wanajukwaa wakati wa kongamano kubwa la wajasiriamali akina mama wa mkoa wa Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mt Paulo Msalaba.


Akitoa maelezo ya awali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wajasiriamali wanawake mkoa wa Dodoma Bi. Maryrobbi Mabhaya alisema tuzo hiyo imetolewa maalum kwa ajili ya kuthamini na kuenzi mchango mkubwa wa mbunge huyo kwa maendeleo yao na hasa katika kuwatafutia fursa na uwezeshwaji kiuchumi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amempongeza Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa karibu na wakinamama katika eneo la uwezeshwaji kiuchumi na akatumia fursa hiyo kuwataka kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hasa katika eneo la kilimo cha mashamba makubwa ya pamoja (Block Farms).


Aidha mbunge huyo amewashukuru wakina mama wa Dodoma kwa kutambua mchango wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuahidi kuja na programu mbalimbali nyingi zaidi za kuwajengea uwezo na kuwawezesha ikiwemo hatua ya sasa ya kutafuta Taasisi ya fedha ambayo itawakopesha akina mama wajane bila riba.













No comments