WANAJESHI WAWILI WA MALAWI WASOMBWA NA MAJI WAKIOKOA WALIOKUMBWA NA KIMBUNGA
Wanajeshi wawili wa Malawi wamesombwa na maji baada ya mashua yao ya uokoaji kushindwa kuhimili kasi ya maji siku ya Jumanne katika eneo la Mulanje kusini, wakiwa katika zoezi la uokoaji wa watu walioathiriwa na Kimbunga Freddy.
Askari hao walikuwa ni sehemu ya wafanyakazi sita waliokwenda kuokoa watu waliokwama baada ya Kimbunga cha Tropiki Freddy kukumba eneo hilo, Waziri wa Serikali ya Mtaa Richard Chimwendo Banda aliambia chombo cha habari cha eneo hilo.
Wanajeshi wengine wawili na raia mmoja walifanikiwa kuogelea na kujiokoa baada ya boti yao kukumbwa na hitilafu ilipokuwa njiani kutekeleza kazi ya uokoaji, Waziri aliiambia Zodiak Online.
Banda alisema mmoja wa askari waliotoweka alionekana kwenye mti na juhudi za kumwokoa zinaendelea.
Kumbunga Freddy, dhoruba iliyovunja rekodi ambayo ilitua katika taifa hilo lisilo na bandari kusini-mashariki mwa Afrika mwishoni mwa juma, imesababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Kituo cha kibiashara cha Malawi, Blantyre, kimeshuhudia vifo vingi, ikiwa ni pamoja na makumi ya watoto. Mamlaka imechelewesha kufunguliwa kwa shule hadi Ijumaa na kutangaza hali ya dharura katika wilaya 10 za kusini ambazo zimeathiriwa zaidi na kimbunga hicho.


Post a Comment