KOCHA YA MONASTR AVUTIWA NA MZEE WA KUTETEMA
Novic Darko, Kocha Mkuu wa AS Monastr ya Tunisia, ameelezea kuvutiwa kwake na mshambuliaji namba moja wa Yanga, Fiston Mayele raia wa DRC.
Akizungumza baada ya mchezo baina ya timu hizo uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kocha huyo alisema Mayele ambaye aliwafungia wenyeji bao la pili, ni mshambuliaji tishio na mwenye uwezo mkubwa wa kupiga mabao na akasisitiza kuwa endapo atapata nafasi ya kuongeza mchezaji, basi Mkongo huyo atakuwa chaguo lake la kwanza.

Post a Comment