POLISI WAWEKWA TAYARI KWA LOLOTE MAMLAKA ZIKIJIANDAA KUMKAMATA TRUMP

Wakati Waendesha Mashtaka wa New York wakijiandaa kumkamata kwa kesi ya Jinai Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump leo Jumanne, polisi wamewekwa kwenye hali ya tahadhari kujiandaa kukabiliana na lolote kutoka kwa wafuasi wake.

Trump anakabiliwa na tuhuma za rushwa wakati wa kampeni za uchaguzi alioshinda wa mwaka 2016, aliyoitoa ili kumziba mdomo mcheza filamu za ngono aliyedaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Vizuizi vya chuma vilikuwa vimewekwa nje ya Mahakama ya Manhattan ambayo ndipo anapoweza kushtakiwa, kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole, katika shauri ambalo linaenda kuandika historia ya kuwa rais pekee wa taifa hilo kubwa duniani kuwahi kufikishwa  mahakamani kwa makosa ya jinai.


No comments