JOSE CHAMELEON AWASHTUA MASHABIKI JUKWAANI, AFANYA TUKIO LA AJABU
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Uganda, Jose Chameleon amewashangaza mashabiki wake na jamii kwa ujumla baada ya kupanda jukwaani na kubusiana kimapenzi na ndugu yake, ambaye pia ni mwanamuziki, Weasal.
Tukio hilo, lililotokea katika tamasha lake kubwa zaidi kuwahi kutokea lililopewa jina la Gwanga Muje wikiendi iliyopita, lilimlazimu mwanamuziki huyo mkubwa Afrika Mashariki kuwaomba radhi mashabiki na jamii kwa jumla.
Msanii Weasal.
Jose alipanda jukwaani na ndugu yake huyo na katika mfululizo wa shoo hiyo, wawili hao walikulana denda kimapenzi, hali iliyoleta sintofahamu kubwa, hasa kutokana na msimamo wa serikali ya Uganda kupinga kwa nguvu zote mapenzi ya jinsia moja.
Haikueleweka mara moja kama jambo hilo lilifanywa makusudi kutetea ushoga, lakini baada ya lawama nyingi mitandaoni, msanii huyo alirusha video katika akaunti yake ya Twitter, akiomba msamaha kwa jambo hilo na kuahidi kutorudia tena.

Post a Comment