CCM MBINGA YAJIPANGA USAJILI WA KIELEKTRONIKI NA ULIPAJI ADA
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma kimejipanga kuhakikisha usajili wa wanachama wapya unafanywa kielektroniki sambamba na ulipaji wa ada.
Hayo yalijiri wakati wa kikao cha kimkakati kilichoongozwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Mary Mwenisongole na Maafisa tehama wa kata zote 48.
Baadhi ya maofisa Tehama wa Kata za Wilaya ya Mbinga wakimsikiliza Katibu wa Wilaya, Mary Mwenisongole.
Lengo la kikao hicho ilikua ni kufuatilia utendaji wa kazi katika vishikwambi (posi) pamoja na kutoa mpango kazi wa mwaka 2023 kwenye upande wa usajili wa Wanachama.
Maofisa Tehama wa Kata za Wilaya ya Mbinga wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa CCM wilaya, Mary Mwenisongole (aliyevaa kofia).
Pamoja na hayo katibu alipata wasaa wa kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wasajili hao kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi sambamba na kupeana mbinu mbalimbali za kuweza kuwasaidia kuongeza ufanisi katika kutekeleza jukumu lao hilo muhimu kwa chama.
Aidha maofisa hao na kiongozi wao walipeana mkakati wa usajili ili kuhakikisha Mbinga inaenda kufanya vyema katika zoezi la usajili wa Wanachama kwenye mfumo sambamba na ulipaji wa ada.

Post a Comment