BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI WATAKA SHERIA YA KINGA KWA VIONGOiZI IONDOLEWE

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) limeshauri kuondolewa kwa sheria ya kinga kwa viongozi ili wasishtakiwe wanapofanya makosa wakiwa madarakani.

Ushauri huo umetolewa mbele ya Tume ya Haki Jinai inayokusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya haki za msingi za raia wa Tanzania.

Viongozi ambao wananufaika na sheria ya kinga ya sasa ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Spika wa Bunge na Naibu wake.

No comments