GIANNI INFANTINO AULA TENA FIFA

Giovanni Vincenzo "GianniInfantino, raia wa Uswisi aliyezaliwa Machi 23, 1970 amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa muda wa miaka minne.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Infantino mwenye umri wa miaka 52, kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ambayo kwa mara ya kwanza aliichukua mwaka 2016 na safari hii amepita bila ya kupingwa kwenye kongamano lililofanyika Kigali nchini Rwanda leo Alhamisi.

Mwanasheria huyo ameiongoza FIFA tangu kuondoka kwa utawala wa Joseph Blatter, mnamo mwaka 2016 na bado anayo nafasi ya kuwania tena mwaka 2027.

Nchi kadhaa za Ulaya, zikiwemo Ujerumani, Norway na Uswidi, hazijafurahishwa na urais wake na zimesema hazitamuunga mkono kikamilifu.


No comments