BOLA TINUBU RAIS MPYA NIGERIA

Asiwaju Bola Ahmed Tinubu, aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama tawala cha All Progressives Congress (APC), ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali nchini Nigeria.

Mahmud Yakub, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Nchini Nigeria (INEC) akimtangaza Tinubu, alisema alipata kura 8,794,726 akimshinda mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Peoples Democratic Party (PDP) aliyepata kura 6,984,520 huku Peter Obi wa Labour Party akipata kura 6,101,533.

Tinubu, gavana wa zamani wa jiji la Lagos anachukua nafasi ya Rais Mahammadu Buhari anayemaliza muda wake.

Hata hivyo uchaguzi huo umelalamikiwa na wapinzani, ambao waliondoka katika Ukumbi uliotumika kutangaza matokeo hayo, wakisema mfumo wa kielektroniki uliotumiwa na tume ya uchaguzi haukuwa na uwazi.

No comments