WASANII NYOTA WATATU WAHUDHURIA HARUSI YA WANANDOA TOKA FAMILIA YA MARAIS ZBR
Wasanii Lady Jaydee, Ali Kiba na Nandy, jumapili ikiyopita walikuwa miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria harusi kutoka familia ya marais wa Tanzania na Zanzibar.
Arafa, binti anayetajwa kuwa ni mtoto wa dadake Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akifunga ndoa na mtoto wa Rais Hussein Ally Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aitwaye Salum.
Marais hao wawili pia walihudhuria sherehe hiyo yenye hadhi ya kirais ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Nishati January Makamba.

Post a Comment