BEI YA PETEOL YAPANDA, EWURA YATOA BEI ELEKEZI YA UKOMO

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa bei elekezi ya bidhaa za mafuta huku ikionyesha mafuta ya petrol yamepanda tofauti na toleo la mwezi Februari.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Mwainyekule, imesema mafuta aina ya petrol yamepanda kwa shilingi 149/lita, Dizeli ikiongezeka kwa shilingi 25/lita na mafuta ya taa yakipanda kwa shilingi 37/lita moja, kwa bidhaa hiyo ambayo itakuwa imeshushwa katika bandari ya Dar es Salaam.

Alisema bei hizo pia zinaweza jupatikana kwa kupiga simu kwa *150*00# kwa mitandao yote ya simu na huduma hii inatolewa bure.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jambo hilo linafanyika kwa kufuata sheria ya mafuta ya mwaka 2015 kifungu cha 166 ambacho kinasema bei za mafuta zitaendelea kupangwa na soko na EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa bei za ukomo.

No comments