ASKARI SHOGA ZANZIBAR KUCHUNGUZWA
Jeshi la Polisi Zanzibar limesema linachunguza madai ya askari wake mmoja kuonekana katika kipande cha video kinachosambaa mitandaoni, akifanya mapenzi ya jinsia moja.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad alisema wameiona video hiyo, lakini haimuonyeshi akiwa amevaa nguo za polisi au akifanya kitendo hicho kituo cha polisi, hivyo wanafanya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kumpima na endapo atathibitika kuwa shoga, atafukuzwa kazi na kisha kupelekwa mahakama ya kijeshi.
Video hiyo ambayo imekua gumzo kubwa mitandaono, inamuonyesha askari huyo akiwa anafanya mapenzi hayo ya jinsia moja na habari zinasema ni mume wa mtu.
Kamishna Hamad pia alisema kufuatia kadhia hiyo, jeshi hilo halipaswi kuhusishwa na vitendo hivyo kwani inawezekana askari huyo alianza kujihusisha na ushoga kabla ya kujiunga na polisi.
Alisema pia watawapima askari wote ili kubaini wanaojihusisha na ushoga.

Post a Comment