ZITTO KABWE AWEKA WAZI NIA YAKE YA KUUTAKA URAIS WA TANZANIA

Zitto Zuberi Kabwe, mwanasiasa kijana ambaye aliwavutia vijana wengi kujiingiza katika siasa kutokana na ushawishi, uwezo wa kujenga hoja, kujiamini na utambuzi wa mambo, ameibuka na kuweka wazi dhamira yake ya miaka yote kwamba anatamani kuwa rais wa Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Zitto ambaye alipata umaarufu mkubwa akiwa Chadema kabla ya kuondoka na kuanzisha chama chake cha ACT Wazalendo, alisema anatamani kuipata nafasi hiyo kupitia mifumo halali ya uchaguzi na kwamba akiipata, ataleta mambo makubwa ya kimaendeleo.

Alisema kikosi kazi kilichopo hivi sasa kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kinashughulika na mambo muhimu, ikiwemo Katiba Mpya, kuruhusu shughuli za vyama vya siasa ikiwemo mikutano ya hadhara na maridhiano ya kisiasa.


No comments