MCHECHU AULA TENA KWA RAIS SAMIA
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Nehemia Mchechu, ameula tena baada ya leo kuteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus, imesema Rais Samia Suluhu Hassan amemteua kushika nafasi hiyo ambayo awali ilishikiliwa na Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Pia Rais Samia amemteua Hamad Abdalah kuwa Mkurugenzi wa NHC akitokea Giamcoafrika.
Aidha Rais Samia amemteua Mussa Mohamed kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), akitokea kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi washirika hilo.
Anachukua nafasi ya James Matarajio ambaye kwa mujibu wa taarifa hiyo atapangiwa kazi nyingine. Teuzi hizo zinaanza rasmi leo.

Post a Comment