MBUNGE ALIYEISHIA LA SABA AJINADI KUTAKIWA NA VYUO VIKUU 11 AKAFUNDISHE UCHUMI
Maajabu hayaishi. Mbunge wa Geita Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi, ambaye elimu yake inafahamika ni ya darasa la saba, amewaacha watu midomo wazi baada ya kudai zaidi ya vyuo vikuu 11 nchini, vinamgombea ili aende kufundisha uchumi!
Musukuma ambaye amekuwa akiwashambulia wasomi mara kwa mara, hivi karibuni aliinasibu kutunukiwa Udaktari wa Heshima, lakini chuo kilichompa heshima hiyo hakijulikani.
Katika mazungumzo yake yaliyonaswa mitandaoni, mwanasiasa huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, alisema anakataa ofa hiyo kwa kuwa anaamini watu watafaidika na 'madini' aliyonayo.
Miongoni mwa PHD zingine zinazowaacha watu midomo wazi bungeni, ni pamoja na ile ya Mbunge wa Morogoro Kusini, Hamisi Tale maarufu kama Babu Tale.

Post a Comment