WATAKA R KELLY ATOKE JELA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 100
Waendesha mashtaka nchini Marekani, wameitaka mahakama kumuongeza kifungo cha miaka 25 jela, mara atakapokuwa amemaliza kikamilifu adhabu yake ya kukaa gerezani kwa miaka 30 kutokana na kesi iliyotolewa hukumu jijini New York.
R Kelly anakabiliwa na kesi nyingine huko Chicago itayotolewa hukumu Alhamis ijayo, na waendesha mashtaka wanataka mwanamuziki huyo aongezewe miaka 25 jela.
Waendesha mashtaka hao wanataka adhabu hiyo kali kwa kile walichosema mwanamuziki huyo ni mtu katili, mnyama na mnyanyasaji mkubwa wa kingono.
R Kelly, mwenye nyimbo nyingi za kuvutia duniani, amekuwa akihusishwa na ufanyaji ngono na wasichana wadogo, kitu ambacho kilifikia tamati mapema mwaka jana alipohukumiwa kwenda jela kwa miaka 30.

Post a Comment