DIAMOND AMEMUOA ZUCHU KWA SIRI? PICHA ZA HARUSI ZATAMBA MITANDAONI
Picha za msanii wa muziki maarufu zaidi nchini, Diamond Platnumz zimezagaa mitandaoni,zikionyesha wameoana na Zuhura Kopa 'Zuchu'.
Diamond ni bosi wa lebo kubwa ya muziki ya WCB na Zuchu ni miongoni mwa wasanii wa lebo hiyo. Wawili hao kwa kipindi kirefu sasa wamekuwa wakizungumzwa kuwa wako katika uhusiano.
Mara kadhaa mama wa binti huyo, Khadija Kopa amekuwa akisisitiza kuwa mwanaye hajawahi kumtambulisha Diamond au mwanaume yeyote kama mchumba wake.
Usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Zuchu alivujisha picha hizo na dada wa Diamond, Esma alikoment katika picha hizo akimuita Bibi Harusi ambapo binti huyo alijibu kwa kuweka alama ya kucheka!!!

Post a Comment