RAIS AKATAZA WANAWAKE NCHI NZIMA KUTOTUMIA JINA LINALOFANANA NA BINTIYE
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Ju, ametoa agizo kwa wanawake wote nchini humo, wenye jina linalofanana na binti yake, Ju Ae kubadili mara moja.
Wanawake wa nchi hiyo inayoongozwa na familia moja kwa miongo mingi sasa, wamepewa wiki moja kutekeleza agizo hilo.
Ju Ae, mwenye umri wa miaka kumi, kwa siku za karibuni amekuwa akionekana akiwa pamoja na baba yake katika matukio mengi ya kitaifa kiasi cha watu kuanza kuhisi huenda ndiye akawa mrithi wake.
Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi wa taifa hilo kutoa agizo kama hilo kwani hata baba yake alitoa agizo kama hilo akikataza kusiwepo na jina kama lake katika nchi hiyo inayoshutumiwa na nchi za Ulaya na Marekani kutofuata haki za binadamu.

Post a Comment