HARMONIZE AMTWISHA MWANA FA ZIGO LA DIAMOND

Siku chache tu baada ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu zaidi kama Mwana Fa, ametwishwa zigo zito.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya mwenye mipasho mingi, Harmonize, anayelalamika kuibiwa fedha zake kutoka mitandao ya kijamii, akiituhunu kampuni ya Wasafi, inayomilikiwa na Diamond kuwa miongoni mwa washirika, amemtaka mkali huyo wa muziki wa kufokafoka kuanza  na suala hilo mara akiingia ofisini.

Harmonize anadai kampuni inayosimamia stahiki zake za muziki ya Ziiki, haijawahi kumpatia fedha zake kwa muda mrefu sasa,kiasi kwamba anahitaji wanasheria wa kumsimamia ili apate anachostahili.



No comments