WANANDOA WAOKOLEWA CHINI YA KIFUSI UTURUKI SIKU 12 BAADA YA TETEMEKO

Mume na mke wameokolewa wakiwa chini ya kifusi katika mji wa Antakya ulio kusini mwa Uturuki, siku 12 baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi katika nchi hiyo na Syria.

Shirika la uokoaji la Uturuki limesema, wanandoa hao walikutwa wakiwa na hali nzuri, na wamesema walimudu kuishi kwa kula wadudu na kunywa mkojo.

Wanasema walishuhudia watoto wao watatu wakifa mmoja baada ya mwingine kitu ambacho hakitakaa kiwatoke katika akili zao.


No comments