KISA MALI, AMUUA MAMA YAKE WA KAMBO, NAYE AUAWA GEITA

Mwanamke mmoja aliyekuwa na ujauzito wa miezi saba, Renata Elias mwenye umri wa miaka 27, ameuawa na mtoto wa mume wake, kwa kile kinachodaiwa kugombea mali.

Mauaji hayo yametokea mkoani Geita ambako kijana huyo akiwa na rafiki yake, walifika nyumbani hapo majira ya saa mbili usiku wakijidai kuangalia tv, lakini muda mchache baada ya mama yake kuingia bafuni kuoga, walianza kumuua kwa kumkata shingo mtoto mdogo wa miaka mitatu kabla ya kumfuata na kumuua mama huyo.

Hata hivyo kufuatia kelele za marehemu wakati wa mauaji hayo, wananchi walisogea na baada ya kuona tukio hilo, walichukua sheria mkononi kwa kuwapiga hadi kuwaua vijana hao.

Mume wa marehemu, aliyetambulika kwa jina moja la Msafiri, naye alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu cha tumbo wakati wa tukio hilo lililoleta simanzi kubwa mkoani humo.

No comments