MWILI WA ATSU WAWASILI GHANA, KUZIKWA KWA HESHIMA ZA KITAIFA

Mwili wa mwanasoka wa kimataifa wa Ghana, Christian Atsu, umewasili nchini Ghana jana Jumapili huku jeneza lake likiwa limefunikwa bendera ya Taifa hilo.

Atsu, aliyekuwa akiichezea timu ya Ligi Kuu Uturuki ya Hayaspor, alipatikana chini ya kifusi cha nyumba aliyokuwa akiishi Jumamosi iliyopita, siku nane baada ya tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo na Syria, ambapo hadi jana watu 45,000 walithibitika kupoteza maisha.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka, jijini Accra, Makamu wa Rais wa Ghana, alisema kipenzi hicho cha wananchi wa Ghana, akiwa ameichezea timu ya taifa mechi 65,  atazikwa kwa heshima zote za kitaifa.

Atsu amewahi pia kucheza England, akizitumikia Everton na Newcastle.

No comments