WANANCHI WA KIPINGUNI A HAWANA IMANI NA WATATHMINI KULIPWA KUPISHA UPANUZI JNIA
Wananchi wa Kipinguni A ambao walifanyiwa tathmini ili kulipwa maeneo yao kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wamesema hawana imani na timu ya utathmini iliyohakiki malipo yao ya fidia, wakidai 'kupigwa'.
Wakazi wa eneo hilo linalokadiriwa kuwa na kaya 885,000, wamesema watathmini hao walitoa malipo ya chini, tofauti na thamni ya sasa ya majengo na mazao yaliyo katika maeneo yao wakati zoezi hilo likifanyika mwaka 1997.
Sophia Waziri, mmoja wa wakazi hao, aliiambia Sauti ya America (Voa) kuwa waliofanya tathmini hawakutoa hesabu sahihi, akitolea mfano ya nyumba ya vyumba vitano, yenye mabanda ya uani, kuthaminishwa kwa shilingi milioni 29 pekee.
Alisema maeneo yao yapo katikati ya jiji, city center, kitu ambacho kama wangeuza kwa mwekezaji wa kuweka kituo cha mafuta, wangelipwa si chini ya shilingi bilioni 2.
"Tunaiomba Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania kutuma watathmini wapya ili waje na hesabu za sasa, kuwaleta watu walewale wanaolalamikiwa siyo sawa,"alisema.

Post a Comment