MWANAFUNZI AJERUHIWA KWA KUIBA MAANDAZI DUKA LA SHULE

Mwanafunzi wa kidato cha nne mkoani Mbeya, amejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na walimu wanne na walinzi wawili, akituhumiwa kuiba maandazi katika duka la shule.

Laurance Mwangake amelazwa katika hospitali ya Ifisi mjini Mbalali, akituhumiwa kuiba maandazi na kuadhibiwa, tukio ambalo Mganga Mkuu wa hospitali hiyo na Kamanda wa Polisi mkoani humo, wamethibitisha.

Inadaiwa Laurance, alinyemelea na kudokoa maandazi hayo na baada ya kubainika, alichukuliwa na kuanza kupewa kipigo, ambacho kimesababisha majeraha kichwani.

Lakini walimu walidai hawakumpiga isipokuwa alitoroka kwa kuruka dirisha kitendo kilichosababisha majeraha hayo.

No comments